SlideShare a Scribd company logo
S
ekta ya kilimo ni sekta inayotegemewa sana katik kukuza
uchumi na kuendeleza maisha ya watanzania walio
wengi. Hata hivyo sekta hii imeendelea kutawaliwa
na wakulima wadogo wadogo ambao ni takribani
asilimia 70 ya watanzania wote. Kwa upande mwingine
kilimo kinachangia kati ya asilimia 10-14 ya hewa ukaa
inayosababisha mabadiliko ya tabianchi na wanaoathirika
zaidi na athari za mabadiliko tabianchi ni wakulima wenyewe
kwa kuwa wao hutegemea kilimo kwa asilimia 100.Tanzania
ina fursa ya kupambana na mabadiliko tabianchi hasa kwa
kuboresha njia za kilimo.
MJUMITA kwa kushirikiana na mashirika ya TFCG, TOAM
na ANSAF wanatekeleza “Mradi wa Mabadiliko Tabianchi,
Kilimo na Kupunguza Umasikini” katika Wilaya ya Kilosa
katika vijiji vya Lunenzi,Ibingu,Kisongwe,Chabima na Mfuruni
na Wilaya ya Chamwino katika vijiji vya Manchali, Mahama,
Nzali Manchali B na Makoja. Lengo la mradi ni kuwajengea
uwezo wakulima wadogo wadogo kupunguza umasikini kwa
kuboresha mbinu za kilimo ambazo zitawasaidia kukabiliana
na athari za mabadiliko tabianchi.
Kwa zaidi ya miaka miwili sasa (toka Oktoba 2012), mradi
umekuwa ukitoa mafunzo ya mbinu za kilimo kwa wakulima
wadogo wadogo hasa mbinu zinazohifadhi rutuba ya udongo,
zinazohifadhi unyevu wa udongo, matumizi bora ya mbolea
za asili, matumizi ya mbegu za asili zilizoboreshwa ambazo
zinakomaa kwa muda mfupi na ambazo zinastahimili ukame,
lakini pia namna ambavyo wanaweza kuyafikia masoko ya
mazao wanayozalisha.
Mbinu hizi zimesaidia kuleta tija kubwa kwa wananchi wengi
ambao wamezijaribu ikiwa ni pamoja na kuongeza faida kwa
wakulima. Mfano, wakulima ambao waliweza kuzitekeleza
vizuri waliongeza uzalishaji kutoka wastani wa magunia 5 kwa
ekari mpaka kufikia wastani wa magunia 15.
Hata hivyo pamoja na mafanikio makubwa ya mbinu hizi mpya
za kilimo kwa wakulima wadogo wadogo katika kupunguza
umasikini na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi,
kumekuwa na changamoto kadhaa zinazowakwamisha
wakulima kunufaika zaidi. Kwa kuwa nyingi ya changamoto za
wakulima zinaweza kutafutiwa ufumbuzi kwa urahisi na utashi
wa Serikali na viongozi wa kuchaguliwa, wakulima kutoka vijiji
vya Kisongwe, Ibingu, Lunenzi, Chabima, Mfuruni, Ludewa
na Mvumi Wilayani Kilosa, walikutana mapema mwezi wa
6 ili kutafakari kwa kina changamoto wanazokabiliana nazo
ili wakati wa kampeni wasisitize wagombea kufahamu
changamoto zao. Katika mkutano huo ambao uliuhudhuriwa
na wataalamu wa wilaya,waheshimiwa madiwani na wakulima
walitoa mapendekezo ya namna ambavyo kila changamoto
waliyoiibua inaweza kushughulikiwa. Changamoto hizi ni
kama ifuatavyo:
♦	 Miundo mbinu mibovu ya barabara na mawasiliano;
Wakulima walio wengi wanaishi vijiji ambavyo bado
havifikiki kirahisi kwa misimu yote ya mwaka na hivyo
kushindwa kupeleka mazao yao kwenye masoko ya
uhakika. Matokeo yake wakulima wadogo wadogo
wamekuwa wakiuza mazao yao kwa walanguzi
wanaotembelea vijiji vyao kwa bei ya hasara na maisha
yao kuendelea kuwa duni kila siku.Aidha vijiji vingi bado
havina mawasiliano ya simu na hivyo wakulima kukosa
fursa ya kufahamu bei ya soko la mazao yao kabla ya
kuyauza kwa walanguzi na hivyo walanguzi kutumia
fursa hiyo kuwalangua wakulima.
♦	 Kucheleweshwa kwa pembejeo za kilimo; Ili
wakulima waweze kuzalisha zaidi na kukabiliana na
athari za mabadiliko ya tabianchi ni muhimu sana kuwa
na pembejeo bora za kutosha na kwa wakati. Asilimia
kubwa ya pembejeo za kilimo ambazo hutolewa na
Serikali huwafikia wakulima zikiwa zimechelewa na
hivyo kutokuwa na msaada wowote kwa wakulima.
♦	 Viongozi kutosimamia sheria na miongozo ya kilimo
na mazingira; Kumekuwa na mapungufu makubwa
katika usimamiaji wa sheria ndogo ndogo za kilimo na
misitu na kupelekea kilimo kufanyika katika maeneo
yasiyotengwa na kusababisha uharibifu wa mazingira
ikiwa ni pamoja na misitu na uharibifu wa vyanzo vya
maji.Uharibifu wa misitu hasa unaotokana na kilimo
UCHAGUZI MKUU NA CHANGAMOTO ZA
WAKULIMA WADOGO WADOGO NCHINI
Je vipi vipaumbele vya wakulima wadogowadogo katika uchaguzi ujao?
Mkulima Bw.Kipara
kutoka kijiji cha
Ibingu amenunua
pikipiki baada ya
kulima nyanya kwa
kutumia mbinu
za kilimo rafiki
na mazingira na
anaitumia kupeleka
mazao yake sokoni.
Mkulima Bw. Ally kutoka kijiji cha Ibingu
akipima nyanya kwenye ndoo ambazo
zinawakandamiza wakulima.
cha kuhama hama kimekuwa kikichangia athari za
mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima wadogo wadogo.
♦	 Wakulima kukosa fursa ya kukopeshwa na taasisi za
kifedha; Wakulima wadogo wadogo wanakosa fursa
ya kupata mikopo toka taasisi mbalimbali za kifedha
ili kuwekeza kwenye kilimo na hii inasababishwa na
kutokurasimishwa kwa ardhi zao na kupatiwa hati miliki.
♦	 Maeneo makubwa ya ardhi kumilikiwa na
wawekezaji wachache; Maeneo mengi ya ardhi
yanamilikiwa na wawekezaji wachache wakiwaacha
wakulima wadogo wadogo wakiwa hawana maeneo
ya kilimo ya kutosha. Ugawaji huo wa ardhi umekuwa
ukifanyika bila kuwashirikisha wananchi wa maeneo
husika na kupelekea migogoro ya mara kwa mara kati
ya wakulima wadogo wadogo na wawekezaji.
♦	 Ongezeko la migogoro ya wakulima na wafugaji:
Kumekuwepo na migogoro ya mara kwa mara
kati ya wakulima na wafugaji inayotokana na aidha
kutokuwepo kwa mipango ya matumizi bora ya ardhi
au kutosimamiwa vizuri kwa mipango bora ya ardhi
na hivyo kupelekea vifo na ulemavu kwa baadhi ya
wananchi. Migororo hii ya ardhi imekuwa ikizorotesha
juhudi za wakulima katika kuongeza uzalishaji na
kupambana na umasikini
Mapendekezo ya wakulima wadogo wadogo
kwa wananchi wanaogombea nafasi mbali
mbali za uongozi katika uchaguzi mkuu.
♦	 Serikali itakayoingia madarakani itoe kipaumbele katika
kuendeleza huduma za jamii vijijini kama barabara,
zahanati, shule, masoko na mitandao ya simu. Vile
vile kiongozi atakayechaguliwa ahamasishe wananchi
kuanzisha vituo vya kuuzia mazao na kusimamia sheria
ndogo za kuzuia wafanyabiashara wasio waaminifu
kutumia vipimo visivyo sahihi vinavyowaibia wakulima
mazao yao na Serikali kutopata kodi stahiki.
♦	 Viongozi watakaoingia madarakani wahakikishe
kwamba bajeti kwa ajili ya kilimo inaongezwa ili kufikia
maazimio ya mkutano wa Maputo (asilimia 10 ya
bajeti ya Serikali ielekezwe kwenye sekta ya kilimo.
Hii itaboresha upatikanaji wa pembejeo za kilimo
kwa wakati, utoaji wa elimu ya ugani kwa wakulima na
utatuzi wa changamoto za masoko.
♦	 Viongozi watakao chaguliwa waweke mkazo katika
kuwajibisha watendaji ambao watashindwa kusimamia
mipango na sheria ndogo za usimamizi wa misitu
na kilimo. Pia elimu ya kilimo na mazingira iendelee
kutolewa kwa wadau mbalimbali ili kila mtu afahamu
wajibu wake na kuutekeleza.
♦	 Viongozi watakao chaguliwa watoe kipaumbele
katika kutengeneza na kuisimamia kikamilifu mipango
ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji, kupima ardhi na
Imeandaliwa na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu
Tanzania (MJUMITA) chini ya “Mradi wa Mabadiliko yaTabia nchi,
Kilimo na Kupunguza umasikini”
Kwa maelezo zaidi wasiliana na:
MJUMITA
Mtandao wa jamii wa Usimamizi wa MisituTanzania (MJUMITA)
S.L.P 21522, Dar es salaam | Simu: +255 22 2669007
Barua pepe: mjumita.org@mjumita.org |Tovuti: www.mjumita.org
wananchi wamilikishwe ardhi zao kisheria. Hii itasaidia
wakulima kuwa na hadhi ya kukopesheka na hivyo
kuendeleza shughuli zao za kilimo na shughuli nyingine
za kiuchumi.
♦	 Viongozi watakao chaguliwa wahakikishe kuwa
michakato ya ugawaji na umilikishaji wa maeneo ya ardhi
kwa wawekezaji inafuata taratibu za nchi, inafanyika
kwa uwazi na wananchi wanashirikishwa kikamilifu
ili kuepuka migogoro mikubwa kati ya wakulima na
wawekezaji, kutokana na wananchi kukosa maeneo
ya kutosha kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine za
kiuchumi..
♦	 Ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji, Serikali
itakayochaguliwa iwekeze katika kuboresha maeneo
yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji ili wafugaji
wabaki katika maeneo yao. Hii ni pamoja na kuweka
miundombinu ya maji na malisho kwenye maeneo ya
ufugaji.
Shamba la mtama katika kijiji cha
NzaliWilayani Chamwino
Mkulima Bi Susan kutoka kijiji cha Kisongwe
ambaye hayupo ndani ya mradi akichuma
mboga ambazo amezipanda kwa kutumia
mbinu za kilimo rafiki na mazingira.
Maharage yaliyopatikana kutokana na
kilimo rafiki na mazingira
Wanachi wakiwa
pamoja na diwani
wa kata ya
Lumuma (Mwenye
Miwani) wakijadili
mambo ambayo
wangependa
yawekwe kwenye
ilani za vyama.
Mkulima Bw.
Kiliani kutoka kijiji
cha Kisongwe
akiwaelekeza
wanafunzi wa shule
ya msingi Lumuma
namna ya kutumia
mbinu za kilimo
rafiki na mazingira
na namna
zinavyoleta tija.

More Related Content

DOC
Maazimio ya asasi zisizokuwa za kiserikali
DOC
District budget analysis study report final
DOC
Research report on economic returns for investing in smallholder farmers (2)
PPT
Mwaka wa pili
PDF
Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...
DOC
PROFILE KIJOGOO
Maazimio ya asasi zisizokuwa za kiserikali
District budget analysis study report final
Research report on economic returns for investing in smallholder farmers (2)
Mwaka wa pili
Risala kwa wananchi kilele wiki ya maji 2013 bulendabufwe bunda iliyosomwa na...
PROFILE KIJOGOO

More from Climate Change Agriculture and Poverty Alleviation in Tanzania (16)

PDF
Final report radio program-ccap- steper consulting co. ltd
DOC
To r for analyzing risks and opportunities of farm inputs
PDF
Tor for assessing impact of radio programmes
PDF
Final report dadp study mjumita consultancy- stephen nyagonde 2013
PDF
Policy Analysis in relation to climate change adaptation, mitigation, agricul...
PDF
Documentation of lessons and the best practice for csa
PDF
Demand and Supply Challenges in Sub-Saharan Africa
PDF
Manual for climate smart agricultural training
Final report radio program-ccap- steper consulting co. ltd
To r for analyzing risks and opportunities of farm inputs
Tor for assessing impact of radio programmes
Final report dadp study mjumita consultancy- stephen nyagonde 2013
Policy Analysis in relation to climate change adaptation, mitigation, agricul...
Documentation of lessons and the best practice for csa
Demand and Supply Challenges in Sub-Saharan Africa
Manual for climate smart agricultural training
Ad

CCAP leaflet.

  • 1. S ekta ya kilimo ni sekta inayotegemewa sana katik kukuza uchumi na kuendeleza maisha ya watanzania walio wengi. Hata hivyo sekta hii imeendelea kutawaliwa na wakulima wadogo wadogo ambao ni takribani asilimia 70 ya watanzania wote. Kwa upande mwingine kilimo kinachangia kati ya asilimia 10-14 ya hewa ukaa inayosababisha mabadiliko ya tabianchi na wanaoathirika zaidi na athari za mabadiliko tabianchi ni wakulima wenyewe kwa kuwa wao hutegemea kilimo kwa asilimia 100.Tanzania ina fursa ya kupambana na mabadiliko tabianchi hasa kwa kuboresha njia za kilimo. MJUMITA kwa kushirikiana na mashirika ya TFCG, TOAM na ANSAF wanatekeleza “Mradi wa Mabadiliko Tabianchi, Kilimo na Kupunguza Umasikini” katika Wilaya ya Kilosa katika vijiji vya Lunenzi,Ibingu,Kisongwe,Chabima na Mfuruni na Wilaya ya Chamwino katika vijiji vya Manchali, Mahama, Nzali Manchali B na Makoja. Lengo la mradi ni kuwajengea uwezo wakulima wadogo wadogo kupunguza umasikini kwa kuboresha mbinu za kilimo ambazo zitawasaidia kukabiliana na athari za mabadiliko tabianchi. Kwa zaidi ya miaka miwili sasa (toka Oktoba 2012), mradi umekuwa ukitoa mafunzo ya mbinu za kilimo kwa wakulima wadogo wadogo hasa mbinu zinazohifadhi rutuba ya udongo, zinazohifadhi unyevu wa udongo, matumizi bora ya mbolea za asili, matumizi ya mbegu za asili zilizoboreshwa ambazo zinakomaa kwa muda mfupi na ambazo zinastahimili ukame, lakini pia namna ambavyo wanaweza kuyafikia masoko ya mazao wanayozalisha. Mbinu hizi zimesaidia kuleta tija kubwa kwa wananchi wengi ambao wamezijaribu ikiwa ni pamoja na kuongeza faida kwa wakulima. Mfano, wakulima ambao waliweza kuzitekeleza vizuri waliongeza uzalishaji kutoka wastani wa magunia 5 kwa ekari mpaka kufikia wastani wa magunia 15. Hata hivyo pamoja na mafanikio makubwa ya mbinu hizi mpya za kilimo kwa wakulima wadogo wadogo katika kupunguza umasikini na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi, kumekuwa na changamoto kadhaa zinazowakwamisha wakulima kunufaika zaidi. Kwa kuwa nyingi ya changamoto za wakulima zinaweza kutafutiwa ufumbuzi kwa urahisi na utashi wa Serikali na viongozi wa kuchaguliwa, wakulima kutoka vijiji vya Kisongwe, Ibingu, Lunenzi, Chabima, Mfuruni, Ludewa na Mvumi Wilayani Kilosa, walikutana mapema mwezi wa 6 ili kutafakari kwa kina changamoto wanazokabiliana nazo ili wakati wa kampeni wasisitize wagombea kufahamu changamoto zao. Katika mkutano huo ambao uliuhudhuriwa na wataalamu wa wilaya,waheshimiwa madiwani na wakulima walitoa mapendekezo ya namna ambavyo kila changamoto waliyoiibua inaweza kushughulikiwa. Changamoto hizi ni kama ifuatavyo: ♦ Miundo mbinu mibovu ya barabara na mawasiliano; Wakulima walio wengi wanaishi vijiji ambavyo bado havifikiki kirahisi kwa misimu yote ya mwaka na hivyo kushindwa kupeleka mazao yao kwenye masoko ya uhakika. Matokeo yake wakulima wadogo wadogo wamekuwa wakiuza mazao yao kwa walanguzi wanaotembelea vijiji vyao kwa bei ya hasara na maisha yao kuendelea kuwa duni kila siku.Aidha vijiji vingi bado havina mawasiliano ya simu na hivyo wakulima kukosa fursa ya kufahamu bei ya soko la mazao yao kabla ya kuyauza kwa walanguzi na hivyo walanguzi kutumia fursa hiyo kuwalangua wakulima. ♦ Kucheleweshwa kwa pembejeo za kilimo; Ili wakulima waweze kuzalisha zaidi na kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabianchi ni muhimu sana kuwa na pembejeo bora za kutosha na kwa wakati. Asilimia kubwa ya pembejeo za kilimo ambazo hutolewa na Serikali huwafikia wakulima zikiwa zimechelewa na hivyo kutokuwa na msaada wowote kwa wakulima. ♦ Viongozi kutosimamia sheria na miongozo ya kilimo na mazingira; Kumekuwa na mapungufu makubwa katika usimamiaji wa sheria ndogo ndogo za kilimo na misitu na kupelekea kilimo kufanyika katika maeneo yasiyotengwa na kusababisha uharibifu wa mazingira ikiwa ni pamoja na misitu na uharibifu wa vyanzo vya maji.Uharibifu wa misitu hasa unaotokana na kilimo UCHAGUZI MKUU NA CHANGAMOTO ZA WAKULIMA WADOGO WADOGO NCHINI Je vipi vipaumbele vya wakulima wadogowadogo katika uchaguzi ujao? Mkulima Bw.Kipara kutoka kijiji cha Ibingu amenunua pikipiki baada ya kulima nyanya kwa kutumia mbinu za kilimo rafiki na mazingira na anaitumia kupeleka mazao yake sokoni. Mkulima Bw. Ally kutoka kijiji cha Ibingu akipima nyanya kwenye ndoo ambazo zinawakandamiza wakulima.
  • 2. cha kuhama hama kimekuwa kikichangia athari za mabadiliko ya tabianchi kwa wakulima wadogo wadogo. ♦ Wakulima kukosa fursa ya kukopeshwa na taasisi za kifedha; Wakulima wadogo wadogo wanakosa fursa ya kupata mikopo toka taasisi mbalimbali za kifedha ili kuwekeza kwenye kilimo na hii inasababishwa na kutokurasimishwa kwa ardhi zao na kupatiwa hati miliki. ♦ Maeneo makubwa ya ardhi kumilikiwa na wawekezaji wachache; Maeneo mengi ya ardhi yanamilikiwa na wawekezaji wachache wakiwaacha wakulima wadogo wadogo wakiwa hawana maeneo ya kilimo ya kutosha. Ugawaji huo wa ardhi umekuwa ukifanyika bila kuwashirikisha wananchi wa maeneo husika na kupelekea migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima wadogo wadogo na wawekezaji. ♦ Ongezeko la migogoro ya wakulima na wafugaji: Kumekuwepo na migogoro ya mara kwa mara kati ya wakulima na wafugaji inayotokana na aidha kutokuwepo kwa mipango ya matumizi bora ya ardhi au kutosimamiwa vizuri kwa mipango bora ya ardhi na hivyo kupelekea vifo na ulemavu kwa baadhi ya wananchi. Migororo hii ya ardhi imekuwa ikizorotesha juhudi za wakulima katika kuongeza uzalishaji na kupambana na umasikini Mapendekezo ya wakulima wadogo wadogo kwa wananchi wanaogombea nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi mkuu. ♦ Serikali itakayoingia madarakani itoe kipaumbele katika kuendeleza huduma za jamii vijijini kama barabara, zahanati, shule, masoko na mitandao ya simu. Vile vile kiongozi atakayechaguliwa ahamasishe wananchi kuanzisha vituo vya kuuzia mazao na kusimamia sheria ndogo za kuzuia wafanyabiashara wasio waaminifu kutumia vipimo visivyo sahihi vinavyowaibia wakulima mazao yao na Serikali kutopata kodi stahiki. ♦ Viongozi watakaoingia madarakani wahakikishe kwamba bajeti kwa ajili ya kilimo inaongezwa ili kufikia maazimio ya mkutano wa Maputo (asilimia 10 ya bajeti ya Serikali ielekezwe kwenye sekta ya kilimo. Hii itaboresha upatikanaji wa pembejeo za kilimo kwa wakati, utoaji wa elimu ya ugani kwa wakulima na utatuzi wa changamoto za masoko. ♦ Viongozi watakao chaguliwa waweke mkazo katika kuwajibisha watendaji ambao watashindwa kusimamia mipango na sheria ndogo za usimamizi wa misitu na kilimo. Pia elimu ya kilimo na mazingira iendelee kutolewa kwa wadau mbalimbali ili kila mtu afahamu wajibu wake na kuutekeleza. ♦ Viongozi watakao chaguliwa watoe kipaumbele katika kutengeneza na kuisimamia kikamilifu mipango ya matumizi bora ya ardhi ya vijiji, kupima ardhi na Imeandaliwa na Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania (MJUMITA) chini ya “Mradi wa Mabadiliko yaTabia nchi, Kilimo na Kupunguza umasikini” Kwa maelezo zaidi wasiliana na: MJUMITA Mtandao wa jamii wa Usimamizi wa MisituTanzania (MJUMITA) S.L.P 21522, Dar es salaam | Simu: +255 22 2669007 Barua pepe: mjumita.org@mjumita.org |Tovuti: www.mjumita.org wananchi wamilikishwe ardhi zao kisheria. Hii itasaidia wakulima kuwa na hadhi ya kukopesheka na hivyo kuendeleza shughuli zao za kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi. ♦ Viongozi watakao chaguliwa wahakikishe kuwa michakato ya ugawaji na umilikishaji wa maeneo ya ardhi kwa wawekezaji inafuata taratibu za nchi, inafanyika kwa uwazi na wananchi wanashirikishwa kikamilifu ili kuepuka migogoro mikubwa kati ya wakulima na wawekezaji, kutokana na wananchi kukosa maeneo ya kutosha kwa ajili ya kilimo na shughuli nyingine za kiuchumi.. ♦ Ili kuepusha migogoro ya wakulima na wafugaji, Serikali itakayochaguliwa iwekeze katika kuboresha maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya shughuli za ufugaji ili wafugaji wabaki katika maeneo yao. Hii ni pamoja na kuweka miundombinu ya maji na malisho kwenye maeneo ya ufugaji. Shamba la mtama katika kijiji cha NzaliWilayani Chamwino Mkulima Bi Susan kutoka kijiji cha Kisongwe ambaye hayupo ndani ya mradi akichuma mboga ambazo amezipanda kwa kutumia mbinu za kilimo rafiki na mazingira. Maharage yaliyopatikana kutokana na kilimo rafiki na mazingira Wanachi wakiwa pamoja na diwani wa kata ya Lumuma (Mwenye Miwani) wakijadili mambo ambayo wangependa yawekwe kwenye ilani za vyama. Mkulima Bw. Kiliani kutoka kijiji cha Kisongwe akiwaelekeza wanafunzi wa shule ya msingi Lumuma namna ya kutumia mbinu za kilimo rafiki na mazingira na namna zinavyoleta tija.